Serikali ya nchi ya Guinea-Bissau imemsimamisha kazi meya wa jiji la Bissau, Luis Ntachama kwa tuhuma za ufisadi wa uuzaji wa ardhi na kushindwa kulipa mafao ya wafanyakazi.

Ntachama amekuwa katika ofisini hiyo tangu Aprili 2021, na ni mwanachama wa Social Renewal Party (PRS), ambacho ni muundo wa muungano wa Rais ukiwa na Viongozi wanazozana na kambi ya Mkuu wa nchi, Rais Umaro Sissoco Embalo.

Kwa mujibu wa agizo la Waziri wa Tawala za Mikoa Fernando Gomes, amesema Ntachama anatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa vya makusudi katika ugawaji wa ardhi ya umma, kutolipa pensheni kwa wafanyakazi wa Manispaa na kuwasimamishwa kazi watumishi wa Manispaa bila ya haki.

Serikali imesema imeamua kumsimamisha kazi Ntachama kuanzia leo Juni 21, 2022, ambaye amekuwa meya wa Bissau tangu 1994 ameteuliwa na serikali.

Meya huyo, amesimamishwa kazi pamoja na washirika wake wawili, Naibu wake wa kwanza na Katibu mkuu wa Taasisi ya Manispaa na sasa nafasi ya Ntachama itachukuliwa na Fernando Mendes, mwanachama wa chama cha kambi ya urais.

Young Africans yaendelea kupeta Ligi Kuu
Ombi la akina Mdee ladunda