Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga amewataka wananchi wanaoishi mjini kuacha tabia ya kukadilia na kutoa michango midogo isiyoweza kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati hususani ujenzi wa madarasa ya shule.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24Media mjini Njombe ambapo amesema kuwa licha ya halmashauri yake kujitahidi kuwapeleka watoto wote katika shule mbalimbali lakini wakazi wa halmashauri hiyo bado hawana mwamko wa kutoa michango.

”Kwa ujumla sisi hapa kwetu hakuna mtoto anayebaki bila kwenda shule, na watoto wote tumewapeleka katika kata zingine, nadhani mpaka mwishoni wa mwezi huu tutakuwa na madarsa ya ziada, lakini tunatakiwa kufanya jitihada ili kukamilisha majengo haya tuliyonayo, niombe na kuwashauri wakazi wa mjini waache kuchangisha michango kama unakwenda kujenga choo huwezi kuchangia shilingi 4000,”amesema Mwanzinga

Aidha halmashauri ya Mji wa Njombe imetoa shilingi Milioni 90 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya Madarasa Kwenye Shule Zake za Sekondari Zilizokuwa na Upungufu wa Madarasa Uliosababisha Baadhi ya Wanafunzi Kukosa nafasi na kulazimika kuwasambaza watoto katika kata mbalimbali.

Hata hivyo, Halmashauri ya mji wa Njombe imefaulisha jumla ya wanafunzi 3001 ambapo kati yao 572 walielezwa kukosa nafasi kutokana na uhaba wa madarasa jambo lililowalazimu kuwapeleka kwenye kata nyingine ambazo hazina upungufu wa madarasa.

 

Bilionea tajiri zaidi duniani ayashindwa mapenzi, aandika ujumbe na mkewe
Wakulima mkoani Njombe watakiwa kuachana na kilimo cha mazoea