Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amesema kuwa hana mpango wa kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2020.

Amesema kuwa anaimani na utendaji kazi wa mbunge wa jimbo hilo, Saed Kubenea hivyo haoni sababu ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha kugombea nafsi hiyo ya ubunge.

Aidha, ameongeza kuwa atawania nafasi ya ubunge endapo litaanzishwa jimbo jipya kwani hadi sasa anaridhishwa na utendaji kazi wa mbunge wa jimbo hilo, huku akisema suala la maendeleo linahitaji mshkamano.

“Mwaka 2020 sioni sababu ya kugombea nafasi ya ubunge kwani majimbo yote yanayoongozwa na upinzani hadi sasa wanafanya kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi katika majimbo yao,”amesema Jacob

Hata hivyo, majimbo yanayoongozwa na wapinzani ni pamoja na Kibamba (John Mnyika), Kawe (Halima Mdee), Ubungo (Saed Kubenea), Kinondoni (Maulid Mtulia), Abdallah Mtolea (Temeke) na Ukonga ni Mwita Waitara.

Video: Rayvany na ngoma yake mpya 'Chuma ulete'
Tamko la Chadema zuio la kongamano Geita