Meya wa Ubungo, Jacob Steven anashikiliwa na jeshi la polisi jijini Dar es salaam kwaajili ya kufanya nae mahojiano ambayo hayakuwekwa wazi kwa wakati huo huku viongozi wengine wa Chadema wakiachwa huru.

Aidha, kukamatwa kwake kumekuja wakati akijiandaa kufanya ziara ya kutembelea Manispaa ya Ubungo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye.

Askari hao wanne wakiwa katika gari aina ya LandCruiser walizuia msafara huo ambao ulipangwa kuanzia katika ofisi za Meya huyo zilizopo Kibamba jijini Dar es salaam na kuomba waondoke nae kwaajili ya mahojiano.

“Tunakuomba uongozane na sisi mpaka kituoni tunamaongezi nawewe yasiyozidi dakika kumi tukiridhika tutakuachia uendelee na shughuli zako unazozifanya,”amesikika askari polisi aliyemfuata.

Zitto ampongeza Rais Magufuli, "Umeitendea nchi haki, hongera sana"
Mchakato Wa Uchukuaji Fomu TFF

Comments

comments