Abdulrazak Gurnah ni mwandishi wa riwaya Mtanzania, anayeishi nchini Uingereza. Alizaliwa Disemba 20, mwaka 1948 visiwani Zanzibar.

Alikwenda Uingereza kama mwanafunzi mwaka 1968, miaka saba baada ya Tanzania kupata uhuru na amekuwa akiishi huko kwa muda mrefu na mpaka sasa ni mwalimu wa fasihi katika chuo kikuu cha Kent.

Alifika Uingereza mwaka 1968 kama mkimbizi baada ya kukimbia Zanzibar kutokana na machafuko yaliyowalenga watu wenye asili ya Kiarabu wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar. Gurnah amewahi kusema, ‘Nilikuja Uingereza wakati ambao maneno kama “asylum-seeker” hayakua yakitumika sana kama wakati huu, watu wengi zaidi wanateseka na kukimbia nchi za kigaidi’

Alipofika Uingereza alianza kusoma kwenye Chuo cha Christ Church College, Canterbury baadaye akahamia Chuo Kikuu cha Kent alipopata Shahada ya Uzamili katika fasihi mnamo mwaka 1982.

Kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka1983, Gurnah alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Bayero mjini Kano, nchini Nigeria na baadae Akarudi uingereza na kuwa profesa wa fasihi hadi alipostaafu

Mbali na kufundisha Gurnah amekuwa akifanya kazi za kuhariri nyaraka mbalimbali, vitabu na majarida na sasa ni mhariri wa jarida la ‘Wasafiri.

Mbali na Tuzo ya mwaka huu 2021 ya Nobel ya Mwandishi Bora wa fasihi inayompa umaarufu Zaidi, Gurnah amewahi kupata tuzo kadhaa huko nyuma kwa sababu ya umahiri wake wa kuandika riwaya zilizosaidia kuleta mageuzi.

Mwaka 1994, akiwa ameanza kufahamika kwa uwezo wake wa kuandika riwaya, alifanikiwa kutwaa tuzo ya Booker Prize for Fiction, iliyoanza kumtambulisha kwenye ulimwengu wa waandishi.

Mwaka 2001 pia haukupita bila bila kwani alifanikiwa pia kutwaa tuzo yake ya pili kubwa ya Los Angeles Times Book Prize (Fiction).

Kati ya tuzo zinazofahamika zaidi alizowahi kupata ni pamoja na ile aliyopata mwaka 2006, ya jumuiya ya madola iliyoitwa ‘Commonwealth Writers Prize (Eurasia Region, Best Book)

Abdulrazak Gurnah anatambulika zaidi kwa namna anavyoamini suala la ukweli na kutopindisha meneno. Alipozungumza na shirika la Habari la BBC baada ya kushinda Tuzo hii ya Nobel Gurnah anasema falsafa ya uandishi wake ni ukweli.

Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Gurnah zinaonyesha mazingira ya pwani ya Afrika ya Mashariki, na wahusika wakuu wa riwaya zake ni wenyeji wa Unguja. Mhakiki wa fasihi Bruce King aliona kwamba Gurnah anaonyesha wahusika wake Waafrika katika uhusiano mpana na Dunia yote, akiwaona kama sehemu za Dunia kubwa inayoendelea kubadilikabadilika. Bruce King, alipomuongelea Gurnah anasema wahusika wake mara nyingi ni watu walioondolewa katika asili zake, wanaokataliwa na jamii na kujisikia kama wahanga wa maisha. Mhakiki Felicity Hand aliona kuwa riwaya za Admiring SilenceBy the Sea na Desertion zote zinajadili hisia za kuwa mgeni na kukosa ndugu zinazotokea kwa watu waliopaswa kuondoka kwao na kukaa ugenini. 

Waandishi wengi wa riwaya, hasa wenye asili ya Afrika, huandika riwaya na vitabu mbali mbali kwa hadithi za kufikirika, lakini uthabiti wa Abdulrazak Gurnah ni kuandika ukweli na mambo mengi halisi.

Anaamini kwamba pamoja na kazi za aina nyingine za kuburudisha, kufundisha na kuelemisha kwa kutumia hadithi mbalimbali, lakini ukweli unapaswa kupewa kipaumbele.

Haitakushangaza kuona riwaya zake nyingi alizoandika kuhusu uhamiaji, alitumia uhusika uliofichua na kuanika uzoefu wa uhamiaji pamoja na maisha ya ujumla ya wahamiaji hasa wanaotoka Afrika na kuingia Ulaya.

Uhamiaji na watu kuyakimbia makazi yao, ama kutoka Afrika Mashariki kwenda Ulaya au ndani ya Afrika ni masuala ambayo karibu riwaya zake zote zimejiegemeza huko. Na humo utabaini kile anachokisema, na kuonekana kama anakosoa lakini anazungumza kilichopo na anachoamini ndio ukweli wenyewe.

Abdulrazak Gurnah, alikuwa tayari amepata sifa kama msomi na mkosoaji wa fasihi wa Kiafrika na alishawahi kuchapisha riwaya tatu kuhusu jamii ya wahamiaji nchini Uingereza mnamo 1994.

Riwaya hizo Memory of Departure (1987), Pilgrims Way (1988) na Dottie (1990), kuhusu masuala ya uhamiaji ikigusia zaidi huko Uingereza, zimemtambulisha zaidi kama mwandishi mzuri.

Riwaya yake ya nne Paradise (1994), iliyoangazia hadithi ya mvulana aliyekulia nchini Tanzania katika karne ya 20 na kushinda tuzo ya Booker na hivyo basi kuzidi kumtambulisha kama nguli wa riwaya.

Riwaya ya Admiring Silence (1996) inamzungumzia kijana ambaye anaondoka Zanzibar na kwenda Uingereza kama mhamiaji ambapo anafika huko anapata mchumba anaoa na baadae anakuwa mwalimu. Ni riwaya ambayo kiuhalisia inayomzungumzia yeye na huo ndio ukweli wenyewe wa fasihi zake.

Kwa sasa Abdulrazak Gurnah anaishi Brighton, mashariki mwa Sussex. Riwaya yake ya hivi karibuni ya Desertion (2005), iliorodheshwa kwenye riwaya zilizowania tuzo ya jumuia ya madola ya mwaka 2006 ‘Commonwealth Writers Prize’ na riwaya nyingine aliitoa mwaka 2011 kwa jina The Last Gift (2011).

Vitabu alivyowahi kuandika na kupata umaarufu ni

2011 – The Last Gift

2007 – The Cambridge Companion to Salman Rushdie

2005 – Desertion

2001 – By the Sea

1996 – Admiring Silence

1994 – Paradise

1993 – Essays in African Literature: A Re-evaluation

1990 – Dottie

1988 – Pilgrim’s Way

1987- Memory of Departure

Ukiwataja manguli wa Riwaya  Nchini Tanzania huwezi kulisikia jina la Abdulrazak Gurnah, kama walivyo manguli wengine akiwemo Shaaban Robert , lakini kwa ushindi huu sasa, amejitambulisha vyema miongoni mwa Watanzania.

Tuzo hii aliyoipata Ya Nobel ambayo imemshikisha kitita cha Zaidi ya dola million moja, ameielekeza kwa Bara la Afrika na waafrika wenyewe.

Polepole avuliwa uongozi
Waziri Gwajima awataka wananchi kuwa makini