Ed Sheeran ni mwanamziki anayefanya vizuri katika muziki wake, na sasa anatamba na kibao chake cha ‘Shape of you’, mwimbo huu unafanya vizuri sana katika orodha ya nyimbo bora kwenye chat ya billboard, 2017.

Ed Sheeran pia ni mahiri katika uandishi wa nyimbo mbalimbali nchini kwao, nyimbo ya ‘shape of you’ aliiandika kwa dhamira ya kumpa mwanamuziki Rihanna ili aufanyie kazi, ila kutokana na mashairi mazuri yaliyopo kwenye wimbo huo, Ed Sheeran akaamua ni vyema akaufanyia kazi yeye mwenyewe, kama inavyoonekana jinsi nyimbo hiyo unavyofanya vizuri katika chat za muziki.

Ukiachana na wimbo huo maarufu wa ‘shape of you’, Ed Sheeran pia ni mwandishi aliyemfanyia kazi nzuri Justin Beiber katika nyimbo ya ‘Love Yourself’ na ‘Cold water’, Beiber aliyoimba na Major Lazor, nyimbo ambazo zimefanya vizuri kipindi chote, na zimeweza kushika nafasi za juu katika nyimbo bora kwenye chat za muziki na katika playlist mbalimbali kama MTV, Trace, BET na Billboard best top 10, 2015.

Kibongobongo mazingira si shwari kwani kila mwanamuziki kwa  asilimia kubwa ni mwaandishi wa nyimbo zake mwenyewe, hali ambayo inapelekea muda mwingine mwanamuziki kushindwa kufikia malengo yake kutokana na kuwa bora katika uimbaji lakini kushindwa kuandika mistari mizuri.

Kulazimisha kufanya vyote kwa pamoja hupelekea mwanamuziki huyu kufeli na kushindwa kukidhi vigezo katika soko la ushindani na ndio maana sasaivi bongo wanamuziki wengi hukimbilia kutoa video nzuri kuziba mapengo, na ndio maana wanamuziki wengi bongo hukimbilia kuanz kutoa video kabla ya audio kukwepa kukosa mashabiki wa nyimbo zao.

Wanawake wenye vitambi hupoteza mvuto, fahamu namna ya kuvikabili
Video: Waziri Mkuu apiga marufuku usafirishaji chakula nje ya nchi, atoa agizo kali