Mshike mshike wa  ya ligi kuu soka nchini England  maarufu kama EPL unazidi kushika kasi katika ligi hiyo ambayo inahusudiwa na mamilioni ya mashabiki wa soka duniani,hii inatokana na ugumu wa ligi hiyo ambao unazidisha burudani kila uchwao.

Gumzo kubwa katika soka hivi sasa ni juu ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa Chelsea,Jose Mourinho ,kufanya vibaya kwa Man United katika michuano ya klabu bingwa pamoja na maajabu yanayofanwa na timu ya Leicester City.

Yote tisa kumi ni juu ya namna ambavyo mshambulijai hatari wa Leicester City Jamie Vardy anavyozidi ‘kutumbua majipu’ ya timu pinzani kila anavyopata nafasi ya kucheza katika kikosi chake.

Vardy ambaye hadi sasa anaongoza katika msimamo wa ligi kuu akiwa na magoli 12 akifuatiwa kwa mbali na mchezaji mwenzake katika timu moja Riyad Mahrez mwenye magoli 7, amekuwa moto wa kuotea mbali hali inayosababisha klabu kubwa mbalimbali kutaka huduma yake katika kipindi hiki cha kuelekea katika dirisha dogo la usajili mwezi january.vardyMathalani klabu kama Chelsea,Man United,Liverpool na Real Madrid ni miongoni mwa klabu kubwa ambazo zimetajwa kufukuzia saini ya mchezaji huyo wa kiamtaifa wa Uingereza.

Pamoja na makali hayo pindi awapo dimbani,Jamie amesema kuwa anayechagiza yeye kuwa katika kiwango cha kutisha ni pamoja na wachezaji wenzake na mbinu toka kwa kocha wake Claudio Reneir.

CHIMBUKO LA JAMIE RICHARD VARDY.

Mchezaji huyu ambaye amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza mara 4 tu katika historia yake,amezaliwa mwaka 1987 katika mji wa Sheffield nchini Uingereza

Akiwa na miaka sita tu,Jamie alijiunga na timu ya mtaani kwake inayoitwa Sheffield Wednesday ambapo alicheza katika timu hiyo kama mshambuliaji hadi mwaka 2002,mwaka uliofuata Jamie alijiunga na Stocksbridge Park Steel ambapo hii ikawa klabu yake ya kwanza katika soka rasmi la ajira tofauti na kule alikotoka ambako alicheza soka la riadhaa.

Akiwa katika timu hiyo,Jamie alicheza jumla ya michezo 107 na kufanikiwa kupachika kimiani jumla ya magoli 66 hali iliyomfanya awe miongoni mwa washambuliaji hatari na wa kutumainiwa na klabu yake.

Cheche za Jamie ziliifanya klabu hiyo kumpandisha hadi timu ya wakubwa ambapo alidumu na timu hiyo hadi msimu wa 2010/11 ambapo alisajiliwa na klabu ya Fc Halifax Town ambapo akiwa hapo alicheza jumla ya michezo 37 na kufunga jumla ya magoli 27.5539974

Akiwa na klabu hiyo Jamie alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa klabu hali iliyozidi kumpa sifa na kumfanya azidi kuzifutia klabu nyingine mbalimbali.

Msimu wa 2011/12 alisajiliwa na klabu ya Fleetwood Town ambapo akiwa hapo alicherza jumla ya michezo 36 na kufunga magoli 31 wasatani wa goli moja katika kila mechi Jamie-Vardy.

Msimu huo ukiwa umemalizika kwa Jamie kuwa mfungaji bora katika klabu yake,klabu ya Leicester City ilivutiwa na huduma zake na kuamua kumsajili kwa dau la pauni milioni 1 katika mkataba wa miaka 3 ambao unakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Akiwa na timu hiyo kabla ya hata kupanda kucheza ligi kuu,alionyesha ni jinsi gani klabu hiyo alilamba dume,kwani katika mechi 113 ambazo ameanza amefunga jumla ya magoli 40.

Jamie akiwa na Leicester City amefanikiwa kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Man United,Ruud Van Nistelrooy ya kufunga katika michezo 11 mfululizo kitu ambacho hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kukifanya.vardy

KUICHEZEA TIMU YA TAIFA.

Kwa mara ya kwanza Jamie aliitwa kuichezea timu yake ya taifa tarehe 21 mwezi wa tano mwaka huu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland,kabla ya kuitwa tena katika kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Euro 2016 dhidi ya Slovenia.

Aidha hadi kufikia sasa mchezaji huyu hajafanikiwa kufunga goli hata moja katika timu yake ya taifa.pia aliitwa katika mechi dhidi ya San Marino na Switzeland.

STAILI YAKE YA MCHEZO.

Wachambuzi wengi wa soka na makocha wa timu mbalimbali wanafananisha uchezaji wa Jamie Vardy na mchezaji wa zamani wa England Salvatore Schillaci ambaye aliichezea Uingereza katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1990.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Jamie hupenda zaidi kucheza soka la nguvu na kushambulia kwa kasi huku akitumia maarifa katika kuwatoka wachezaji na mabeki wa timu pinzani.

MAISHA BINAFSI YA JAMIE VARDY.

Inaelezwa kuwa Jamie ni moja kati ya wachezaji ambao hawana matukio ya kuhuzunisha,japo taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa alihusika katika kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya raia mmoja wa Japan ambapo amwita jina la ‘jap’ ambalo lilitafsiriwa kama ni ubaguzi kwa mtu huyo.

Kufuatia kitendo hiko klabu yake ilimlima faini na kumpa adhabu nyingine ambazo zilitokan an kukiri kutoa kauli hiyo kwa mjapani huyo wakati akiwa klabu yeye na rafiki yake

Mbali na hayo mchezaji huyo ambaye kwa sasa anapokea mshahara wa wiki wa pauni 45,000,kabla ya kujihusisha moja kwa moja na soka la ushindabi,anaripotiwa kuwa amewahi kuhudhuria mafunzo ya uuguzi mwaka 2007

Aidha mapema hivi karibuni Jamie alifungua academy aliyoipa jina la V9 ambayo itakuwa na lenmgo la kuwakutanisha wachezaji wote ambao wanaanza soka bila ya kuwa ndani ya mfumo wa academy kama ambavyo yeye alianza soka la mitaani

 

MAFANIKIO BINAFSI

Moja kati ya mafaniko aliyoyapa ni pamoja na kuibuka mfungaji bora katika ligi daraja ya pili Championship wakati akiichezea klabu yake ya sasa kabla haijapanda ligi kuu,lakini mafanikio yake ya hivi karibuni ni pamoja na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi novembar ya ligi kuu soka UIngereza huku akiwabwaga washindani wake mahiri kama Harry Kane

Cosmas Cheka Ashindwa Kutamba Ulaya
Pep Guardiola Ajisogeza Taratibu Etihad Stadium