Kocha kutoka nchini Ufaransa Sebastian Serge Louis Desabre ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwaniwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, katika kipindi hiki ambacho benchi la ufundi la Msimbazi halina kiongozi (Kocha Mkuu).

Benchi la ufundi la Simba SC, liliachwa bila kiongozi (Kocha Mkuu) majuma mawili yaliyopita baada ya kocha Sven Vandenbroeck kusitisha mkataba wake na kutimkia nchini Morocco kujiunga na FAR Rabat.

Kwa siku zaidi ya tatu sasa Sebastian Serge Louis Desabre aliezaliwa Valence, Ufaransa Tarehe 2/8/1976 amekua akitajwa kuwa sehemu ya wanaofikiriwa sana na viongozi wa Simba SC, kubebeshwa jukumu la ukuu wa benchi la ufundi klabuni hapo.

Desabre mwenye umri wamiaka 44, ana historia ya kuvutia katika ukunzi wa soka ambapo kati ya mwaka 2006- 2010 alifundisha klabu ya ES Cannet-Rocheville ya ufaransa, baada ya kufanya vizuri klabuni hapo akahamia ASEC Mimosas ya ivory coast kwa miaka miwili, kisha 2012 akaingia nchini Cameroon kuinoa timu ya Cotton sports, huko hakukaa sana na ndipo maboss wa Tunisia wakampenda.

Wakahitaji huduma yake mwaka 2013 -14 akainoa klabu ya Esperance de Tunis, kabla ya kuhamia Recreativo do Libolo ya nchini Angola, mwaka 2015,

Mwaka 2016 akajiunga na Dubai CSC na wala hakudumu, kisha akajiunga na Waarabu wenye fedha wa  JS SOURA kule algeria.

Mwaka huo huo akajiunga na Wydad  AC ya Morocco anapocheza msuva hivi sasa. Kisha akafungashiwa virago na kujikuta ISMAILY ya nchini Misri kwa kina Himid Mao.

2017 ulikua mwaka wa neema kwake kwa kusaini kandarasi ndefu na shirikisho la soka Uganda FUFA ili kuinoa timu ya Taifa kwa dau la dola elfu 25 kwa mwezi. Sawa na milioni 58 na ushee za kitanzania.

Tarehe 17 November 2018 Uganda wakafuzu Afcon kwa kuwafunga Cape Verde, kwa kiwango cha timu yao, Uganda ikaorodheshwa kwenye timu 5 bora za kiume Afrika za kiume kwenye tuzo za mwaka 2018. Lakini baada ya kufungwa na  senegal july 5 2019  walitolewa.

Na mkataba wa Desabre ukavunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili. Hakukaa na njaa jamaa huyu, tarehe 8 mwezi wa 7 mwaka 2019 alitangazwa kama kocha mkuu wa Pyramids Fc inayoshiriki ligi kuu Misri. Na januari 2020 akarudi zake wydad Ac ya Morocco.

Huko kote hajawahi kulipwa mshahara chini ya milioni 45.  Hivi sasa anafundisha klabu kongwe sana nchini ufaransa, klabu ya Chamois Niortais inayoshika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa ligi hyo.

Alifanikiwa kutwaa vikombe zaidi ya 7 kwenye vilabu tofauti.

Kama simba watamlipa pesa atakayotaka basi ataweza kuyarudisha makalinya simba klabu bingwa, Huyu ni zaidi ya Sven.

JKT yasitisha mafunzo
Daktari: Carlinhos 'SAFI', Yacouba 'BADO'