Mfalme wa Thailand, Maha Vajiralongkorn amemuoa mmoja kati ya askari waliokuwa wanamlinda, Jenerali Suthida na kumpa hadhi ya Malkia Suthida.

Tangazo la uamuzi huo wa Mfalme limewekwa kwenye Gatezi la Kifalme na kueleza kuwa sherehe rasmi za ndoa ya kifalme zitafanyika Mei 4-6, 2019.

Mfalme Vajiralongkorn alitawazwa kuwa mfalme wa Thailand baada ya kifo cha baba yake, Bhumibol Adulyadej kilichotokea Oktoba 2016, ikiwa ni miaka 70 ya utawala wake.

Mwaka 2014, Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai kuwa naibu kamanda wa kikosi chake cha ulinzi binafsi.

Wakati huo kulikuwa na tetesi kuwa Mfalme ana uhusiano wa kimapenzi na Suthida lakini ikulu ya kifalme haikuutambua uhusiano huo kati yao.

Desemba 2016, Suthida alipandishwa cheo kuwa Generali. Mwaka 2017 alipewa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi cha karibu zaidi cha ulinzi binafsi wa mfalme.

Malkia huyo mpya alizaliwa Juni 3, 1978 akipewa jina la Suthida Tidjai. Alisoma katika Chuo Kikuu cha  Assumption kilichoko Bangkok, akichukua masomo ya sanaa ya mawasiliano akimaliza mwaka 2000. Kwa mujibu wa gazeti la Thai Rath, alianza kazi yake ya kwanza kama mfanyakazi wa ndege wa Shirika la Ndege la Thai, kabla ya kujiunga na kitengo cha kumlinda Mwana wa Mfalme  Vajiralongkorn ambaye hivi sasa ni Mfalme.

Wapiga umbea kutozwa faini na kuokoteshwa takataka masaa 3
Video: Waigizaji 10 Matajiri zaidi Duniani