Mfalme wa Oman, Sayyid Qaboos bin Said Al Said amesema kuwa anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuongeza uwekezaji katika viwanda,

Ujumbe huo wa Mfalme wa Oman umewasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohammed Hamad Al Rumhy aliyeongozana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman, Salem Ben Nasser Al Ismaily na Naibu Waziri wa Utalii, Maitha Saif Majid, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Rumhy ambaye ameongozana na watu zaidi 300 waliokuja nchini kwa meli ya Mfalme wa Oman amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman hususani katika masuala ya uchumi, ambapo Oman inabadilishana uzoefu na Tanzania kuhusu biashara ya mafuta na gesi

Aidha, amesema kuwa Oman itajenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea katika ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo, pia viwanda vya mazao na kununua mazao ya wakulima na itawekeza katika uchakataji wa madini ili kuongeza thamani.

“Mhe. Rais tunataka kushirikiana nanyi kuendeleza ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo, tunataka Bagamoyo isiwe eneo la bandari tu, bali pia liwe ni eneo ambalo tutajenga viwanda mbalimbali, tuzalishe mbolea na tununue mazao ya wakulima na kuyasafirisha, sisi tupo tayari na kesho tunakwenda kuangalia eneo hilo ili kazi zianze mara moja,”amesema Dkt. Rumhy

Alicho andika Tundu Lissu kwa mara ya kwanza
Jose Mourinho aikana kauli yake