Mfalme Salman wa Saudi Arabia amemchagua mwanae Mohammed bin Salman kuwa mrithi wa kiti cha ufalme akimuondoa wadhifa huo binamu yake, Mohammed bin Nayef.

Kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo, mteule huyo pia anapata nafasi ya kuwa Naibu Waziri Mkuu huku akiendelea na nafasi yake kama waziri wa ulinzi.

Aidha, kwa muujibu wa kituo cha runinga cha nchi hiyo, mfalme huyo wamemvua Pince Mohammed bin Nayef cheo cha kuwa mkuu wa mambo ya usalama wa ndani ya nchi.

Mfalme Salman mwenye umri wa miaka 81, alivikwa taji la ufalme wa Saudi Arabia Januari 2015 baada ya kifo cha kaka yake, Abdullah bin Abdul Aziz.

Hatua ya kuteuliwa kwa Prince Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 kuwa mfalme ajaye kumeelezwa kuwa ishara ya mabadiliko makubwa kwa kizazi cha vijana.

Muigizaji maarufu wa Afrika Kusini Apigwa Risasi
Chuji Wa Polisi Morogoro Ajisogeza Mtibwa Sugar