Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mfanyabiashara Romani Shirima (74) ambaye ni mkazi wa Moshi Mjini amejiua kwa kujimwagia mafuta ya petrol na kisha kujilipua kwa kiberiti nje ya nyumba yake.

Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano asubuhi na kwamba bado kiini halisi hakijathibitika ingawa kumekuwa na maelezo mengi. Alisema kuwa jeshi hilo tayari limeanza uchunguzi ili kubaini chanzo chake.

Taarifa zilizotolewa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo, zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alijifunika blanketi na kujimwagia mafuta ya petrol mwili mzima kabla ya kuwasha kiberiti na kujimaliza mapema asubuhi nje ya jumba lake.

Imeelezwa kuwa huenda madeni na msongo wa mawazo vikawa chanzo cha maamuzi ya kujiua kwa mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mmiliki wa shule ya Sekondari ya Merinyo.

Wizara ya Elimu: Mabilioni yaandaa hafla hewa, Jengo hewa Dodoma
Lissu aimwaga tena Serikali Mahakamani