Katika hali isiyo ya kawaida, msichana mmoja mfanyakazi wa kampuni ya Usangu Logistics Ltd, amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya saba ya Jengo la Habour View Tower mapema leo.

Binti huyo aliyetajwa kwa jina la Redna Raphael alijirusha kutoka ghorofani muda mfupi baada ya kuzungumza na simu yake ya mkononi, hali inayodaiwa kuwa huenda ni kutokana na kutofautiana na mpenzi wake kupitia mawasiliano hayo.

Imeelezwa kuwa binti huyo aliyenusurika alikimbizwa katika hospitali ya Mnazimmoja jijini humo na anaendelea na matibabu.

Chanzo: Mwananchi

Masharti Ligi Kuu Duru La Pili
Mmiliki wa Jamii Forums arejeshwa Rumande