Mfanyakazi wa bendi ya Beyonce anamtuhumu mwimbaji huyo kwa uchawi uliokubuhu na unyanyasaji wa kingono.

Kimberly Thompson ambaye alikuwa anafanya kazi ya kupiga ngoma kwenye bendi ya Beyonce kwa kipindi cha miaka saba, amefungua kesi mahakamani ambapo nyaraka za mashtaka zimemuelezea mwimbaji huyo kuwa alitumia nguvu za giza kwa mambo mbalimbali pamoja na kumnyanyasa kingono.

Katika nyaraka hizo ambazo zilishuhudiwa na ‘The Blast’, Kimberly anadai kuwa Beyonce amekuwa akitumia uchawi kudhibiti hali yake ya kifedha pamoja na wafanyakazi wake.

Aidha, alimtuhumu mwimbaji huyo kwa kudukua mawasiliano yake ya simu na kumuua paka wake.

  

Hivyo, pamoja na mambo mengine, Kimberly aliiomba Mahakama kutoa amri ya kumzuia Beyonce kumsogelea au kumfuatilia.

Hata hivyo, mambo hayakwenda sawa ambapo Septemba 19, mahakama kuu ya Los Angeles iliyakataa maombi ya awali ya mlalamikaji.

Imeelezwa kuwa Mahakama hiyo itasikiliza sehemu nyingine ya maombi ya mlalamikaji Oktoba 11 mwaka huu.

Beyonce bado hajazungumzia suala hilo, na wakati huu anaendelea kufanya ziara yake ya ‘On The Run II’ nchini Marekani akiwa na mumewe Jay Z.

Paul Pogba aponda mfumo wa Jose Mourinho
Babajide Ojo kurudi Afrika

Comments

comments