Mfanyakazi wa shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) mkoani Shinyanga, Bupe Mwakibibi (48) ameuawa kwa kupigwa na jiwe kichwani na mume wake, Shyrock kimaro (48) ambaye ni dereva wa pikipiki za biashara maarufu bodaboda mkazi wa kata ya Ibadakuli, mkoani humo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani humo, Alchelaus Mutalemwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Miti mirefu mjini Shinyanga.

Mtelemwa amesema kuwa wanamshikilia Kimaro kwa kufanya shambulio hilo la kumpiga mkewe kwa jiwe kichwani upande wa kushoto na kumsababishia kifo hapo hapo.

Aidha, chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na wao kutengana na marehemu ambapo kabla ya mauti haija mkuta  alimfuata mtuhumiwa kwa ajili ya matumizi na mahitaji ya shule ya mtoto, baada ya kupokea simu mtuhumiwa aliwasili nyumbani akiwa amelewa, walipokuwa hawaelewani ndipo alipo muangusha chini kisha kumpiga jiwe kichwani.

Marehemu ameacha watoto wanne ambao wawili alizaa na mtuhumiwa huku kaimu kamanda amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mehdi Benatia aitwa kuikabili Cameroon, Tunisia
Al Ahly kupinga adhabu ya Walid Azaro

Comments

comments