‘Mzizi wa fitina’ kati ya bondia Mfaume Mfaume na Keisi Ali umekatwa rasmi usiku huu, ukimshuhudia Mfaume akiibuka mshindi kwa alama katika pambano lililokuwa na ufundi wa hali ya juu.

Pambano hilo ambalo lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano la Hassan Mwakinyo na Bondia Mfilipino, Tinampay lilikuwa la kusisimua, huku Mfaume akimpiga chini Keisi katika raundi ya nane.

Hata hivyo, Keisi alifanikiwa kuamka haraka na akaweza kuendelea na pambano ingawa alikuwa ameshaumizwa.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa pambano hilo, Mfaume alikuwa amebadilika akipunguza mbwembwe kwani Keisi alionesha kuwa amejiandaa vizuri na pambano.

Katika pambano lingine, Twaha Kiduku alifanikiwa kumpiga bondia wa Afrika Kusini kwa TKO, baada ya muamuzi kusimamisha pambano alipoona mfululizo wa masumbwi ulioporomoshwa na Kiduku.

Hata hivyo, bondia huyo wa Afrika Kusini alionesha kutokubaliana na uamuzi huo na kulalamika akieleza kuwa anaamini kulikuwa na upendeleo kwani bado alikuwa na nguvu.

Endelea kufuatilia Dar24 tutakupatia matokeo ya pambano kati ya Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay linaloanza muda mfupi ujao.

BREAKING: Hassan Mwakinyo ampiga Tinampay
Matajiri wazawa wa Makete watakiwa kurudi kuwekeza kwao

Comments

comments