Bingwa wa Mkanda wa WBF Bondia Mfaume Mfaume, amefichua siri ya ushindi wake dhidi ya Bondia kutoka nchini Misri Abdelmonem Ahmed Sayed Mohamed, aliyemchakaza usiku wa kuamkia Jumamosi (Julai 02).

Mfaume alimbamiza mpinzani wake katika pambano la Ubigwa wa WBF lililounguruma Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kwa KO, ambayo iliwashangazwa wadau wengi wa Masumbwi waliofuatilia Pambno hilo.

Bondia huyo kutoka Gym ya Nacoz amesema siri kubwa ya kupambana na kushinda pambano hilo la kimataifa, ni kufanya mazoezi kwa kujituma na kuweka malengo ya kushinda katika ardhi ya Tanzania.

Amesema alifanya mazoezi kwa miezi mitatu mfululizo bila kuchoka, kwa kutambua mpinzani wake alikua na viwango vya hali ya juu, kutokana na alivyomfuatilia katika mapambano yake ya nyuma.

“Kushinda mkanda wa WBF sio jambo ndogo na watu wanaona mpambano ulikuwa mwepesi wengine wanasema nilipigana na mlevi wanasahau huyu ni bondia mzuri kutoka Misri.”

“Na pia hata mimi nilikuwa mazoezi kwa miezi mitatu nimejifungia nikifanya mazoezi, sikutakata tamaa, nilifahamu ukubwa na uwezo wa mpinzani wangu, nilimfuatilia katika mapambano yake ya nyuma na kubaini udhaifu wake, ndio maana nimeshinda.” Bondia Mfaume Mfaume

Mfaume Mfaume alikua sehemu ya mabondia wa Tanzania ambao walikua hawajapanda ulingoni kwa kipindi kirefu kabla ya kukutana uso kwa macho na Bondia Abdelmonem Ahmed Sayed Mohamed, usiku wa kuamkia Jumamosi (Julai 02).

Mtuhumiwa mauaji watu saba Kigoma adakwa
Kega ‘amuwashia moto’ Gachagua