Uongozi wa klabu ya Young Africans umesema mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo utakamilishwa mwezi Mei.

Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini wamekuwa na shauku kubwa kuona jambo hilo likitokea.

Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela amewataka Wanachama wa klabu hiyo wakae tayari kupokea mabadiliko hayo. Tumeunda Kamati ambayo inasimamia mchakato huo, tunashukuru kila kitu kinaenda sawa,” Amesema Mwakalebela.

“Tumekuwa tukipokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali. Muhimu zaidi tumepata nafasi ya kwenda kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa”. Lengo letu ni kuwa na mfumo ambayo utaifanya Young Africans isimame na kuweka historia ya Mafanikio”.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo mwaka uliopita, Dk Mshindo Msolla alitangaza suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kuwa kipaumbele chake cha kwanza.

Hii si mara ya kwanza kwa Young Africans kujaribu kubadili mfumo wake wa uendeshaji kuwa kampuni. Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 Young Africans imejaribu mara kadhaa bila ya mafanikio, mivutano baina ya wanachama ikikwamisha zoezi hilo.

Lakini hitaji la mabadiliko wakati huu limekuwa kubwa miongoni mwa Wanachama wa klabu hiyo.

Kama mpango huo utafanikiwa, Dk Msolla ataingia kwenye historia ya klabu hiyo kwa kufanikiwa kumaliza mchakato huo ambao watangulizi wake hawakufanikiwa kuukamilisha.

Buriani Radomir Antic
Maradona awashauri mastaa wa soka