Kampuni ya DataVision International imezindua mfumo mpya wa ADA-LIPA unaomuwezesha mzazi au mlezi kumlipia ada ya shule mwanafunzi kupitia mtandao wowote kwa simu ya kiganjani.

Mfumo huo wa ADA-LIPA unamuwezesha mzazi au mlezi kulipa kidogo kidogo kwa kudunduliza kiwango chochote cha fedha wakati wowote endapo tu shule au chuo imejiunga na mfumo huo unaomuwezesha mzazi kujitengenezea Kibubu cha malipo ya Ada ya mwanafunzi hadi pale atakapokamilisha kiwango kamili cha malipo ya ada kinachohitajika.

Katika mfumo huo mzazi/mlezi atafanya malipo yake kwa kutumia nambari ya  shule na akaunti ya mwanafunzi kwenda kwenye shule husika moja kwa moja kwa makato nafuu ya shilingi 1000 tu kwa viwango vyote (Kuanzia TZS 10,000 hadi TZS 3,000,000). Aidha, faida kubwa ya mfumo huu wa AdaLipa unasaidia kuokoa muda mwingi ambao angeweza kuupoteza mzazi /mlezi kwenda benki kufanya malipo ya ada.

Pia faida nyingine ya kutumia mfumo huo wa AdaLipa ni urahisi wa huduma yenyewe ambapo mzazi au mlezi hutumia simu yake ya mkononi kwa kufanya malipo ya kiwango fulani cha fedha wakati wowote na mahali popote alipo kwenda moja kwa moja kwenye benki ya shule husika.

Akizungumza na Dar24 Media, Afisa wa masoko wa AdaLipa, Ibrahim Stephen amesema, “Mfumo wa AdaLipa unazingatia hali halisi ya majukumu ya mzazi ukiachana na kulipa ada ya mwanafunzi tu, hivyo tumemtengenezea mzazi kibubu kupitia mfumo huu wa Ada lipa ili aweze kulipa kidogo kidogo kadri awezavyo kabla ya ukomo wa malipo ya ada kwa kudunduliza.

Kuanzia shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo sasa wanaweza kunufaika kwa kujiunga na mfumo huo.

Jiunge sasa na mfumo huo kupitia tovuti hii: http://adalipa.co.tz/login/register

 

 

Wafanyabiashara 10 wakamatwa sakata la watoto kuuawa Njombe
Mkuu wa Majeshi Sudan Kusini ashtakiwa kwa uhaini

Comments

comments