Shirika la utafiti wa masuala ya kiuchumi na hisa ‘Moody’s’ limesema kuwa mfumo wa kutumia benki za Kiislamu katika biashara umekuwa ukiongezeka duniani kote katika miaka ya hivi karibuni na hasa barani Afrika.

Mfumo huo wa benki hutumia mali kama msingi wa kufanyia biashara, na haulipishi au kutoza riba na hauwekezi kwenye biashara zinazo fahamika kama haramu katika dini ya Kiislamu kama vile ya pombe, nyama ya nguruwe au kamari.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kwamba Waislamu wengi wanaacha kutumia benki za kawaida na kujiunga na benki hizo za Kiislamu.

Kwa upande wake, Mkuu wa mfumo wa benki wa Kiislamu kwenye benki ya First National ya Afrika Kusini, Amman Muhammad amesema biashara imenawiri barani Afrika kutokana na ongezeko la Waislamu barani humo.

Majaliwa apokea ripoti ya ajali ya MV. Nyerere
Wema: Nimefunga jalada la utoto, nimefunga jalada la ujinga, nimekuwa mpya