Kiungo kutoka nchini Ufaransa Tiemoue Bakayoko ameondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkopo, ambao utamuwezesha kucheza ligi ya Sirie A hadi mwishoni mwa msimu wa 2018/19.

Chelsea wamethibitisha kuondoka kwa kiungio huyo waliemsajili msimu uliopita akitokea AS Monaco ya nchini kwao Ufaransa, na wanaamini akiwa AC Milan atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara, tofauti na mazingira ya Stamford Bridge ambayo hayakumpa nafasi hiyo.

Ujio wa meneja mpya Maurizio Sarri umethibitisha nafasi finyu kwa kiungo huyo kucheza katika kikosi cha kwanza, jambo ambalo pia limechangia kuondoka kwake magharibi kwa jijini London.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, amekamilisha usajili wa mkopo ambao umeigharimu klabu ya AC Milan Euro milioni tano, na kama ataonyesha kiwango cha kuridhisha hadi mwishoni mwa msimu, huenda akasajiliwa jumla kwa ada ya Euro milioni 35.

Tangu alipotua Chelsea msimu wa 2017/18, Bakayoko alicheza michezo 29 ya ligi ya soka nchini England na kufunga mabao mawili pekee.

Simon Mignolet kuondoka Anfield
IGP Sirro apongeza hali ya utulivu uchaguzi mdogo wa marudio