Wajanja wa mjini Milan nchini Italia (AC Milan), wapo tayari kumuachia mshambuliaji wao kutoka nchini Colombia Carlos Arturo Bacca Ahumada itakapofika mwezi januari mwaka 2017.

Kocha wa AC Milan Vincenzo Montella ameweka dhamira hiyo, kufuatia mfumo anaoutumia kwa sasa kutotoa nafasi kwa Bacca kucheza kwa uhuru anapokua uwanjani, hivyo ameona kuna umuhimu wa kumruhusu kuondoka.

Klabu ya SSC Napoli inayoshiriki ligi ya nchini Italia (Serie A), imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Hata hivyo huenda ikapata upinzani kutoka kwa West Ham, Sevilla pamoja na PSG ambazo ziliwahi kuonyesha dhamira ya kumsajili wakati wa majira ya kiangazi.

Klabu hiyo zinadhaniwa huenda zikaibuka tena katika kinyang’anyiro cha kumuwania Bacca, kutokana na hitaji la mtu muhimu katika safu zao za ushambuliaji.

Bob Bradley: Donald Trump Ataivurugia Marekani
#HapoKale