Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi nchini utashuka kutoka asilimi 9.8 Desemba mwaka jana hadi asilimia 8.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa hii leo Januari 18, 2023 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa wakati wa Kikao kazi cha Waandishi wa Habari, kilichowajumuisha washiriki toka Benki Kuu ya Tanzania.

Amesema, “Matazamio yetu yanaonyesha kuwa mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi utashuka kwa asilimia 8.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu (Januari hadi Machi), ikilinganishwa na asilimia 9.4 katika kipindi cha Desemba, mwaka jana.”

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa.

“NBS tumekuwa tukifanya matazamio ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni sahihi kama tulivyofanya katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022,” amefafanua Dkt. Chuwa na kuongeza kuwa kwasasa mfumuko wa bei nchini ni asilimia 4.3 kiwango ambacho kitaendelea kudhibitiwa.

Akizungumza na Dar24 Media hivi karibuni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alibainisha kuwa kufikia mwezi Machi Mwaka, 2023 bei ya bidhaa za Kilimo pia zitapungua kwa kiwango kikubwa kutokana na uwepo wa Mvua na uhakika Mavuno.

Waziri afariki katika ajali ya chopa
Wanne Simba SC kuikosa Mbeya City