Kamishna msaidizi wa jeshi la Magereza mkoani Ruvuma, Richard Nyivwe amethibitisha kifo cha mfungwa mmoja aliyefahamika kwa jina la Treson Manyika baada ya kupewa msamaha wa Rais.

Nyivwe amesema, Mnyika alikuwa miongoni mwa wafungwa 181 katika gereza la Mahabusu Songea waliopata msamaha huo, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana.

“Treson Mnyika ambaye bahati mbaya usiku wa kuamkia leo (jana), Mwenyezi Mungu amemchukua, ametangulia mbele ya haki. kwamaana hiyo wafungwa ambao wametoka rasmi wamekuwa 179 baada ya wale wawili mmoja kutoka kwa rufaa na mmoja amechukuliwa na mwenyezi Mungu” Amesema Nyivwe.

katika hatua nyingine mfungwa katika gereza la Ruanda jijini Mbeya, Mernad Abraham aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya ubakaji ambaye alihukumiwa jela mika 30 mwaka 2000 aliomba kurudishwa gerezani kwani hana pakwenda.

Rais Magufuli Juzi katika maadhimisho ya mika 58 ya Uhuru wa Tanganyika alitangaza msamaha kwa wafungwa 5,533 waliopo katika magereza mbalimbali kote nchini.

Nyumba za kulala wageni 'guest house' zachangia mfumuko wa bei
Shinyanga: Wasichana waogeshwa dawa kuvutia wanaume