Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa ametoa siku tatu kwa wamiliki na waendeshaji wa jengo la Mkuki house lililopo eneo la Kamata barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam kujitokeza na kujieleza na kulipa deni la shilingi milioni 270 wasipofanya hivyo jengo hilo litafungwa.

Ameyasema hayo mapema hii leo mara baada ya kufanya ziara katika jengo hilo kwaajili ya kujionea utendaji kazi wake na kutaka kujua ni kwanini uongozi huo haujalipa deni kwa Halmashauri hiyo kwa muda wa miaka miwili mfululizo.

Aidha, Mgandilwa ametoa muda huo wa siku tatu kwa mwekezaji huyo kufika ofisini kwake, kujieleza na kulipa pesa yote wanayodaiwa zaidi ya milioni 270 na kuwa endapo akikahidi agizo hilo hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufungwa kwa jengo hilo na kumwondoa mwekezaji huyo.

Hata hivyo, Mgandilwa ameendelea na ziara yake ya kutembelea wafanyabiashara, wawekezaji na vitega uchumi mbalimbali vilivyopo chini ya manispaa ya Kigamboni ili kujionea uendeshaji wake na kutaka kujua kama taratibu za nchi zinafuatwa ikiwemo kulipa kodi.

JPM azindua Viwanda vitatu mkoani Pwani
Shaa aziota tuzo za ‘Grammy’