Mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Chinaka Adoezuwe mwenye miaka 26 ameuawa kwa kupigwa na risasi na mteja wake.

Mganga huyo ambaye ni raia wa Nigeria alikuwa akijidai kuwa ana nguvu za kuzuia risasi.

Imeelezwa kuwa alijinasibu kuwa ana uwezo kuzuia risasi ambapo alimuagiza mteja wake ampige risasi wakati amevaa dawa hizo za kuzuia risasi shingoni ili kumthibitishia mteja wake kuwa ana uwezo huo kitu ambacho kilipelekea kukatisha uhai wake.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini humo limemkamata mteja huyo kwa madai ya mauaji na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Siku za hivi karibuni nchini Nigeria kumetokea Waganga wengi wanaodai kuwa wana nguvu za kuzuia risasi.

Serikali ya Nigeria imeingilia kati na kuwakamata wote wanaoshiriki katika majaribio hayo ya kutafuta dawa za kuzuia risasi.

Brazil kumkosa Danilo kwenye kombe la dunia
Video: Mambo mazito ya wastaafu kwa JPM, Lugola atoa maagizo mazito saba

Comments

comments