Polisi wilayani Mpigi wanamshikilia mzee, Vincent Ssenonga  mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mganga wa kienyeji kwa kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa mwenyewe baada ya kuwatimua wake zake sita na kuishi na binti huyo tangu akiwa na miaka 13.

Mzee huyo anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Buwama, ambapo polisi wameeleza kuwa taarifa juu ya mzee huyo walizipata kutoka kwa wasamaria wema.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mzee huyo amekuwa akimnyanyasa binti yake na  kumgeuza mke wake, aliyeanza kufanya naye ngono tangu akiwa na miaka 13 mpaka sasa ana miaka 20, na sasa wamezaa wana watoto watatu.

“Kumuoa na kumtesa mtoto wake mwenyewe, kiasi kwamba hampi chakula na huduma za afya, hatukuweza kuvumilia na kwenda kumchukua huyu mzee. Tumeambiwa kuwa amemtumia huyu binti kwa miaka 7 sasa tangu akiwa na miaka 13, na tunachunguza taarifa kuwa amemuambukiza HIV”, amesema Bwana Jospeh Kakama ambaye ni polisi wa zamu wa kituoni hapo.

Naye mwenyekiti wa kijiji Bwana Robert Ssemuju amesema mganga huyo alikuwa akiishi na binti yake huyo pekee, baada ya kuwapa talaka wake zake sita, na watoto wake kutawanyika kutafuta maisha huko Kampala na sehemu zingine.

Hata hivyo mzee uyo amekuwa akimtishia binti yake asizungumze chochote kwa ndugu, jirani namarafiki yake juu ya vitendo anavyomfanyia, lakini kutokana na afya yake kudhoofika binti huyo ameamua kufunguka ili asaidiwe yeye na watoto wake watatu alaiozaa na baba yake.

 

Taifa Stars kuondoka Machi 22, Twiga Stars yaingia kambini
Mahakama Vuga yaipiga kalenda tena kesi ya kulawiti