Baada ya Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), kusema kuwa alipewa milioni 40 na aliyekuwa mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa ili amsaidie kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.

Mwenyekiti wa taasisi inayojihusisha na utawala bora ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja, amesema kuwa kauli ya Mbunge huyo haina ukweli wowote.

Mgeja ameyasema hayo Mkoani Tabora alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kauli ya Bulembo si ya ukweli wala haina mashiko yoyote bali ni kutaka kujionyesha msafi kwa wananchi.

“Kwa mtu aliye makini hawezi kuamini kwamba Lowassa alimpa fedha ili amsaidie kwenye kampeni, bali anachofanya Bulembo kwa sasa ni propaganda ya mwendelezo wake wa kila siku wa kumdhihaki, kumdhalilisha na kumkejeli Lowassa,”amesema Mgeja.

Hata hivyo, amesema kuwa kama anaamini kuwa alipewa fedha hizo, basi awataje majina na wengine waliompa msaada wa mamilioni kwa ajili ya uchaguzi.

Pluijm Atuma Salamu Jangwani na Msimbazi
Hans Poppe Aeleza Sababu Ya Simba Kuwa Pamoja