Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amemtaka Kamanda wa Polisi mkoani humo kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwanga na Askari wa kituo kidogo cha polisi  Nyumba ya Mungu na Lang’ata Wilayani kutokana na tuhuma za rushwa dhidi yao.

Mghwira ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Hadhara katika Kata ya Lang’ata, Wilaya ya Mwanga, ambao umehudhuriwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  Humphrey Polepole, na viongozi wengine wa chama na Serikali.

Amesema Askari hao wamekiuka taratibu na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa, hatua ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika jitihada za kudhibiti uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu.

Ameendelea kueleza kuwa Askari hao wamejianzishia vituo vyao vya ushuru na kuanza kukusanya mapato yatokanayo na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu,ambalo lilifungwa baada ya kukithiri kwa uvuvi haramu na samaki kupotea.

“Naomba niseme Askari wa Lang’ata na Nyumba ya Mungu mmenikwaza,kwani kituo chenu kipo juu na mtu hata awe mfupi kunizidi anaweza kuona mazingira yote ya Bwawa na kuona wavuvi haramu,lakini wao huwa hawawaoni,  hii ni hatari sana,naomba RPC uwaondoe mara moja na kuwachukulia hatua,” amesema Mghwira.

Aidha, Mghwira ambaye alitangaza kulifungua Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa Muda, amesema Serikali ilikuwa na nia njema kulifunga Bwawa hilo, lakini Askari wamepoteza malengo ya Serikali na kukwamisha mpango  wa kuacha samaki wawe wakubwa.

Kwa upande wakeKatibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema Serikali haitawavumilia Askari au watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuchafua utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya Tano.

Video: Lugola amzukia Lugumi, Askofu atikisa viongozi, taasisi kwa utapeli
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 22, 2018