Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England, Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata uraia wa Israel.

Amesema kuwa amefikia hatua hiyo mara baada ya kucheleweshewa viza yake kutoka nchini Uingereza huku ikihusishwa na mgogoro wa Kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.

Mgogoro huo umechagizwa zaidi mara baada ya jasusi wa zamani wa Urusi, Sergei na binti yake Yulia Skripal kupewa sumu nchini Uingereza.

Aidha, Viza ya Abromovich ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki chache zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo, Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United 1-0

 

 

 

LIVE: Misa ya Kuagwa kwa Marehemu Bilago Bungeni Jijini Dodoma
Mvutano mkali watokea kuhusu mazishi ya Bilago, Chedema wasusia Gari

Comments

comments