Wakati ambapo timu ya kampeni ya CCM inamvaa Edward Lowassa na Ukawa, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Monduli, Namelock Sokoine amecheza ‘fair’ play na kumsifia mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema.

Akiongea hivi karibuni katika mkutano wa Kampeni jimboni humo Namelack alisifia utendaji kazi wa Lowassa ambaye alimtaja kama mwalimu wake wa masuala ya siasa na kusisitiza kuwa uhuisiano wao hauwezi kuvunjwa kwa tofauti za harakati za kisiasa kwa kuwa urafiki wa familia zao umejengwa katika misingi imara.

“Uhusiano kati ya familia ya Edward Lowassa na Edward Moringe Sokoine umejengwa katika misingi imara isiyoweza kutetereshwa na masuala ya kisiasa au harakati,” alisema Namelock.

Aidha, Namelock alisifu kazi iliyofanywa na wabunge wengine waliotangulia wa jimbo la Monduli akiwemo baba yake mzazi, Marehemu Edward Moringe Sokoine.

Mara kwa mara katika kampeni zake, Namelock amekuwa akijinadi kuwa ndiye anayefaa kuvaa viatu vya Lowassa katika jimbo hilo.

Jana, Lowassa akiwa katika mkutano wa kampeni Monduli, alieleza kuwa ingawa yeye ndiye aliyemshauri Namelock kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, alimtaka pia kukihama chama hicho na kumfuata Chadema la sivyo hataweza kumsapoti kwa kuwa hayuko naye kwenye basi moja. Hivyo, Lowassa alimtambulisha mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Julius Kalanga kama mtu anayefaa kuchukua nafasi yake kwa sasa.

 

Makala: Dk. Magufuli, Dk. Slaa Wameungana Rasmi Kimkakati Kuung'oa Mbuyu
Stars Kuanza Kusaka Tiketi Ya Urusi Kesho