Mgombea udiwani Kata ya Buhangaza, Muleba (Chadema), Athanasio Makoti aliyekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Februari 2, mwaka huu amepatikana akiwa hajitambui katika barabara ya Hospitali ya Kagando.

Hayo yameelezwa na Chadema mara baada ya kumpata mgombea huyo ambae amekuwa haonekani kwa muda wa takribani siku 3.

Imeelezwa kuwa mgombea huyo alipotea alipokuwa akitokea Bukoba mjini kwenda nyumbani kwake Kijiji cha Buhangaza na kutekwa na watu wasiojulikana.

Tukio hilo limetokea kipindi cha Kampeni za ubunge na udiwani zikiendelea katika Kata ya Buhangaza wilayani Muleba.

Chadema.jpg

Viongozi wa NASA wazidi kunaswa na Polisi
Ndugulile: Mama wajawazito wanapaswa kupata huduma za matibabu bure

Comments

comments