Mgomo wa walimu unaoendelea nchini Kenya umepelekea serikali ya nchi hiyo kuzifunga shule zote.

Wizara ya elimu imeandika barua rasmi ya uamuzi wa serikali kuzitaka shule zote zifungwe hadi pale zitakapotangaziwa tena. Hata hivyo, wanafunzi wanaosubiri kufanya mitihani ya darasa la nane pekee mwaka huu ndio walioruhusiwa kuendelea na masomo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu nchini humo amethibitisha kuwa wamepokea barua hiyo ya wizara ya elimu na kueleza kuwa walikuwa wameishauri serikali kuchukua hatua hiyo mapema.

Wakati hali hiyo ikiendelea, Mahakama nchini humo inatarajiwa kutoa uamuzi wake hivi karibuni kuhusu uhalali au ubatili wa mgomo huo ulioitishwa na walimu nchi nzima wakidai nyongeza ya mshahara.

Serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa haina fedha za kutekeleza matakwa ya walimu hao.

Alichofanya Tibaijuka Baada Ya Mpiga Debe Wake Kuteleza ulimi...
Baba Yake Kim K Aliyejigueza Kuwa Mwanamke Ashindania Tuzo Na Malkia Elizabeth