Serikali ya Kenya  jana Aprili 7, 2020 imetangaza wagonjwa wapya 14 na kufanya idadi ya maambukizi ya Corona nchini humo kufika 172 huku Katika wagonjwa wapya waliotangazwa wanne walisafiri hivi karibuni kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu (UAE) na Marekani.

Waathirika hao Wengine 10 ni miongoni mwa waliokuwa wakifuatiliwa na timu za Uchunguzi za Wizara ya Afya.

Waziri wa Afya pia ametangaza kuwa wagonjwa watatu wameruhusiwa baada ya majibu yao kuthibitisha kuwa hawana tena maambukizi na kufanya idadi ya waliopona kufikia 7.

Waziri huyo amesema ni muhimu kwa kila Mkenya kuvaa barakoa, huku akisisitiza kuwa Serikali haitosita kuchukua tahadhari zaidi ili kudhibiti maambukizi ya Virusi hivyo.

Rais Trump aitupia lawama WHO
Corona: Marekani yapata vifo zaidi ya 1500 kwa siku moja

Comments

comments