Naibu waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema kuwa serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo kwa wananchi katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki tofauti na baadhi ya watu wanavyoeneza propaganda juu ya kile kilichotekelezwa katika jimbo hilo.

Mgumba ambae ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa katika Kata ya Kidugalo na Ngerengere mkoani Morogoro.

Amesema kuwa hivi sasa wananchi pamoja viongozi wa CCM katika Jimbo hilo wanatakiwa watembee kifua mbele kutokana na yale yalitokelezwa na serikali ya awamu ya tano chini dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yeye akiwa Mbunge wa Jimbo hilo la Morogoro Kusini Mashariki.

Kuhusu Barabara amesema kuwa hivi sasa barabara nyingi zinapitika amabzo zilikuwa changamoto hapo awali hali iliyaofanya wanachi kuteleza shughuli za zao za kimaendeleo licha ya kuwepo changamoto ndogongo katika baadhi ya barabara ambazo serikali imekuwa ikizitatua kwa kwa wakati.

Pia wamefanikiwa kudhibiti mapato ya halmsahauri ya Wilaya ya Morogoro ambayo yalikuwa yanapotea mikono mwa wachache,ujenzi wa Kiwanda cha kucahata mazao jamii ya mikunde ambacho ni pekee kwa Tanzania Nzima,pia kujengwa kwa kiwanda Kikubwa cha sukari cha Mkulazi kutafungua fursa kubwa ya ajira kwa wakazi wa jimbo hilo na maeneo mengine.

Ujenzi wa Hospital ya Wilaya,na kuhamishwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mogororo kwenda Mvua yote hayo ni moja ya mafanikio amabyo yamepatikana katika serikali ya awamu ya Tano.

Ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Morogoro kusini Mashariki kwa ushirikiano wao walioutoa katika kipindi ambacho alikuwa mbunge wa Jimbo hilo

Abdul Nondo atangaza kumrithi Zitto jimbo la Kigoma Mjini
'Top 5' wagombea urais Zanzibar