Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema Kiungo kutoka nchini Mali Sadio Kanoute anaendelea vizuri.

Kanoute alilazimika kutolewa kwa msaada wa Machela, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars, uliopigwa jana Ijumaa (Februari 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mgunda ametoa uhakika wa hali ya Kanoute, alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi (Februari 04), kuhusu maandalizi ya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Al Hilal ‘Omdurman’ ya Sudan, utakaopigwa kesho Jumapili (Februari 05), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Mgunda amesema Kiungo huyo alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo leo, lakini amesisitiza hakuumia kwa kiwango kikubwa, licha ya kutolewa kwa msaada wa Machela.

“Kanoute anaendelea vizuri na leo amekwenda kufanyiwa uangalizi zaidi, hakuumia sana lakini ninajua huenda kukawa na hofu kwa sababu alitolewa kwa msaada wa Machela.”

“Tunaamini atakuwa sawa na ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kwa michezo inayotukabili hivi karibuni.” amesema Mgunda

147 JKT wakutwa na VVU
Kocha wa Singida Big Stars aitamani Simba SC