Mkuu wa Mkoa Lindi, Godfrey Zambi amefanya ziara ya siku moja Wilayani Ruangwa ambapo amekagua miradi mbalimbali ikiwepo ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Mnacho pamoja na Ujenzi waZahanati ya Kijiji cha Nandagala,Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi

image003

Mh.Zambi akikagua choo cha awali kilichoanguka.

image001

Vyoo vipya vilivyojengwa.

Aidha amektana na alengwa wa Mradi wa Kaya masikini chini ya ufadhili wa TASAF III katika Kijiji cha Mitope na baadae kuhutubia kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Ruangwa ili kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Katika Mkutano Huo,Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi amewataka Walengwa wa Mradi huo kuhakikisha wanatumia Malipo wanayolipwa na TASAF Kuweza Kujiwezesha kuwa na miradi itakayowezesha Jamii Kujikwamua.

image017

Pia amemwagiza Mratibu wa TASAF kuwafuatilia na kuwasimamia walengwa ili wazitumie fedha kwa malengo husika na sio kwa kunywea pombe.

Vilevile watendaji wa Kata na Vijiji wameagizwa kuhakikisha walengwa wa mradi wawe ni wale wanaotakiwa na si vinginevyo kwani kumekuwepo na malalamiko la watu wenye uwezo kuingizwakwenye malipo Huku masikini wakiachwa.

Aidha walengwa wameshauriwa pia kujiunga katika vikundi ili waweze  kuanzisha SACCOS kwaajili ya kuweza kukopeshana.

Mwisho Mkuu wa Mkoa aliwapongeza Walengwa wa Mradi kwa TASAF kwani wapo ambaowamefanikiwa kununua mabati, kujenga vyoo, na kununua mifugo kama kuku na bata.

image012

Ujenzi waZahanati ya Kijiji cha Nandagala ukiwa unaendelea.

Nuhu Mziwanda na tattoo mpya ya mrembo mwingine
Video: Waziri ameitaka Muhimbili kutoa maelezo baada ya taarifa zilizotolewa na gazeti Mwananchi