Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu ), Jenista Mhagama ameitaka (MIVARF) kuongeza thamani ya biashara za mifugo Wilayani Longido.

Ametoa agizo hilo baada ya kukagua soko la kimkakati lililojengwa na serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Program ya miundombinu ya masoko, uongezaji thamani na huduma za kifedha vijijini (MIVARF).

Aidha, Soko hilo la kimkakati limeingiza mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106 kwa mwaka 2016/17, na kusaidia wilaya hiyo kuweka rekodi ya kuingiza mapato ya bilioni 1.3 kwa mwaka.

Hata hivyo, MIVARF ni Programu ya Miundombinu ya Masoko na Huduma za kifedha vijijini, iliyobuniwa mwaka 2011 na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na inatekelezwa katika mikoa 29 nchini.

 

Kili Stars kuikabili Z’bar Heroes, balozi akishudia
Majaliwa afanya ukaguzi wa makazi ya makamu wa Rais