Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu). Jenista Mhagama amefanya ziara ya siku moja jijini Dar es salaam, kwa lengo la kukagua miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja na kutaka kujua mikakati ya kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa jijini humo.
 
Katika ziara hiyo, Mhagama ametembelea wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam hususani katika maeneo ambayo mkoa huo umeboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko.
 
Maeneo aliyoyatembelea ni pamoja na Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni na mfereji wa Mtoni kwa Azizi Ally. pamoja na kuridhishwa na jitihada zilizofanywa na mkoa huo za kuboresha miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko.
 
“Nimeridhishwa na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya uongozi wa Dkt. Joh Pombe Magufuli za kuboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko, na nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote zinavyo jitahidi kujenga uwezo wa kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa. lakini pamoja na jitihada hizo ninge penda kuishauri na kuielekeza kamati na Mkuu wa mkoa ayasimamie maelekezo yangu.”amesema Mhagama
 
Aidha, Mhagama ameiagiza Kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa kusimamia suala la uharibifu wa mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2015.
 
  • Basi la Rungwe Express lapata ajali mbaya mkoani Morogoro
 
  • Polisi Dar yaua majambazi 6
 
  • Serikali yazionya NGOs, yaanza kuzichunguza kimyakimya
 
Hata hivyo, ameitaka kamati hiyo kusimamia suala la usafi wa mitaro, mifereji na mito iliyopo jijini Dar es salaam, ambayo hujaa maji wakati wa msimu wa mvua kutokana na uchafu na takataka zilizotupwa katika mifereji na mitaro hiyo

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 30, 2018
Polisi Dar yaua majambazi 6