Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa ili liweze kudumisha amani na utulivu huku akiupongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kufanya hivyo.

Ametoa pongezi hizo alipokutana na uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Mjini Dodoma ili kujadili na kuipongeza serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

“Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo,”amesema Mhagama

Amesema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wa dini na kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli katika kufikia azma yake ya  ‘Tanzania ya Viwanda’

Hata hivyo, kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini, Arnoid Manase ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.

DRC yagoma kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa
Urusi yaionya Marekani, yaapa kulipiza shambulio lolote