Katibu Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha ifikapo mwezi Machi, 2021 Machinjio ya Vingunguti yawe yameanza kufanya kazi hata kama ujenzi wake ukiwa bado haujakamilika.

Nyamhanga ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kukagua hatua iliyofikia ya ujenzi wa machinjio hayo ambapo alibaini hadi sasa 98% imefikiwa hadi kukamilika kwake.

“Kiwango cha kutoa huduma ya machinjio hii kwa kiasi kikubwa kimeshakamilika hivyo ianze kufanya kazi kwa kuchinja wanyama wachache mpaka hapo itakapokamilika kwa 100%,” amesema Nyamhanga.

Machinjio hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchinja Ng’ombe 1,500 pamoja na Mbuzi na Kondoo 3,000 kwa siku.

Saudia yakanusha Salman kuhusika na kifo cha Khashoggi
Mhandisi Sanga awapa RUWASA siku 60