Serikali nchini, imememuagiza Mhandisi wa Maji Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja maji yaanze kutoka katika jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa na kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Agizo hilo, limetolewa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati alipotembelea miradi ya maji iliyopo jimboni humo na kusema ndani ya siku hizo thelathini, pia mkandarasi ajitahidi kusimamia ujenzi, ukarabati na kusambaza sehemu za kuchotea maji, ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji jimbo la kibakwe.

Amesema, “Niwaombe radhi wananchi na niwaombe sana Tusitafute mchawi, Hawa wataalamu wetu ndio wanatakiwa kutumia maarifa yao kutekeleza mradi huu kwa kuzingatia hali ya udongo wa eneo hili.”

Hata hivyo, Waziri Aweso amewaahidi wana Kibakwe kuwa Serikali itatimiza wajibu wake na hakuna changamoto yoyote zaidi ya wataalamu kutimiza wajibu wao, ili kuwawezesha kupata Maji safi, salama na yenye kutosheleza.

TBS na TMEA 'waweka Bil. 9 mezani' ubora wa bidhaa
Serikali kuandaa utaratibu ukodishaji wa ardhi