Watu tisa akiwemo Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia wametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za ujangili nakuhusika katika kuitungua helkopta ya doria katika pori la akiba Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu, tukio lililosababisha kifo cha rubani wa helkopita hiyo, Rodgers Gower.

Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi hilo chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana, kwa kushirikiana na wananchi pamoja na uongozi wa TANAPA.

Kamanda Mambosasa alieleza kuwa watuhumiwa hao ambao mingoni mwao yumo mganga wa jadi waliokuwa wakiwasaidia katika imani za kishirikina ili wasikamatwe, walikutwa na silaha pamoja na meno ya tembo na wote walikiri kuhusika katika tukio hilo.

Aliwataja watu hao kuwa ni Iddi Mashaka ambaye ni Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Intelijensia ambaye anadaiwa kuwa kinara wa mpango huo.

Wengine ni Shija Mjika, Njile Gonga, Mhazabe, Masasi Mandago pamoja na Dotto Pangali, ambao ndio walihusika kutungua helkopta hiyo. Mbali na hao, wengine ni Mapolu Njige  ambaye ni mganga wa jadi aliyekuwa anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga, Dotto Huya, Pamoja na Mange Balumu.

 

 

 

Mwenyekiti wa Majaji Wastaafu amtetea Rais Magufuli katika hili
Chui avamia shule katika jiji alilodhalilishwa mwanafunzi mtanzania nchini India