Mhubiri mmoja nchini Rwanda amejikuta matatani baada ya kuhubiri kuwa wanawake ni chanzo cha uovu, alipokuwa katika kipindi cha redio.

Mhubiri huyo anayejitabaisha kuwa ni wa imani ya Kisabato (Seventh Day Adventist), Nicolas Niyibikora aliwaeleza wasikiliza kuwa wanawake wametokana na ‘upendeleo wa Mungu’ na kwamba hakuna kitu chema ambacho utakikuta kwa mwanamke.

“Kama unasoma Biblia, nani ameleta dhambi duniani? Aliuza. “Sio mwanaume,” alijibu mwenyewe.

Mahubiri hayo ya Niyibikora yaliamsha hasira za wanaharakati wanaotetea haki za wanawake nchini humo ambao wamezitaka Mamlaka za vyombo vya habari na wizara ya mambo ya ndani kumchukulia hatua kwani anahubiri chuki dhidi ya wanaewake.

Katika mkutano na vyombo vya habari, taasisi ya wanawake ya Pro-Femme Twese

Hamwe nchini humo ilionya kuwa mahubiri ya namna hiyo yanaweza kuleta chuki na migogoro kwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Taasisi kadhaa zimewasilisha malalamiko yao dhidi ya mahubiri hayo kwa Tume ya Vyombo vya Habari ya Rwanda (RMC), ambayo imeahidi kujadili suala hilo wiki ijayo.

Katibu Mtendaji wa RMC, Emmanuel Mugisha ameiambia New Times kuwa redio aliyoitumia mhubiri huyo italazimika kujieleza.

Makanisa ya kisabato nchini Rwanda yamefanya jitihada za kujitenga na Niyibikora ambaye miaka mitano iliyopita aliwahi kuvuliwa uongozi na kutengwa.

Al-Shabaab yaendesha mashindano ya wazee kupiga risasi
Vita ya dawa za kulevya yamponza Durtete