Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imemuhukumu Jumanne Hussein [36] mkazi wa Ughaugha mkoani Sinngida kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kukutwa na nyara ya serikali ambayo ni meno mawili ya tembo yenye thamani ya shilingi million 34,785000.

Hukumu hiyo imetolewa leo juni 16,2021 mbele ya  Hakimu wa Mahakama hiyo Victory Kimario baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri dhidi ya mshitakiwa na mashahidi wanne kati ya saba,  na kuwa mahakama hiyo inamtia hatiani kwenda kutumikia miaka 20 jela .

Kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi wanyamapori ya namba 5 ya mwaka 2009 na kifungu namba 60 [2] cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 kama ilivyo fanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Kwa upande wa mwendesha mashtaka wa serikali Rusticus Mahundi aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo kwani kosa alilotenda linaadhari katika uchumi na kwamba iwefundisho wa watu wengine.

Awali mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la stendi ya mabasi Kateshi wilaya ya Hanang mkoani Manyara akiwa amebeba meno mawili ya tembo katika mfuko aina ya salfeti huku akichanganya na mihogo bila kuwana kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori  Tanzania.

Tanzania, Marekani kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza
TBS waanza ukaguzi wa magari nchini