Septemba 11, 2001 ilileta mabadiliko makubwa nchini Marekani ambapo ilishambuliwa na mtandao wenye msimamo mkali wa Kiislamu, al-Qaeda, baada ya kuteka nyara ndege nne na kuzitumia kama makombora dhidi ya maeneo maalumu ya Marekani.

Katika shambulio hilo takriban watu 3,000 waliuawa na Marekani ilijibu janga hilo kupitia oparesheni iliyoitwa ‘vita dhidi ya ugaidi’ iliyojumuisha uvamizi wa nchi mbili na kusabisha vifo zaidi.

Rais wa Marekani Joe Biden Katika hotuba iliyotumwa mitandaoni, amesema kuwa pamoja na hisia kali za umoja wa kitaifa, baada ya tarehe 11 Septemba 2001, Marekani imeshuhudia pia ushujaa kila mahala, hata kwa sehemu usizotarajia.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Jen Psaki, amesema Rais Biden na mkewe, watakwenda kutoa heshima zao, kwa wahanga wa mashambulizi hayo, katika maeneo matatu yalikofanyika ambako ni New York City, Penn-sylvania, na Pentagon.

Mashambulizi hayo ya kigaidi kwa kutumia ndege za abiria, ndiyo pekee yaliyowahi kufanywa na maadui wa kigeni ndani ya ardhi ya Marekani, katika historia ya taifa hilo lenye nguvu kubwa za kijeshi ulimwenguni, na iliyatumia kama sababu ya kuvamia Afghanistan na Iraq.

Mbunge atimiza ahadi ya ujenzi Biharamulo
Dube kuikosa Heseed FC