Waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amefafanua jinsi serikali ya awamu tano ilivyoboresha sekta ya elimu kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu

Amesema serikali ya awamu ya tano imehakikisha inatatua changamoto za walimu mashuleni ikiwemo changamoto ya kukosa vifaa vya kutumia ambapo kila mwezi serikali inatenga bilioni 24 za kitanzania kuziba pengo la michango isiyokuwa na maelezo kwa wazazi.

“Mtoto wa kitanzania akizaliwa kwenda shule sio hiari ya mzazi ni lazima, Serikali imeamua kuwekeza kwenye elimu na serikali inataka kujilizisha kila anaezaliwa anapata elimu ni lazima na ndio maana Rais alipoingia madarakani mwaka 2016 alifuta michango yote ya hovyohovyo ili kumuwezesha hata yule ambaye hana kipato kikubwa anaenda shule”. Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha serikali imeongeza shule za msingi kutoka shule 16899 hapo awali na kufikia shule za msingi 17804, Kwa shule za sekondari kutoka 2015 kulikuwa na shule 4708 na kufikia shule 5330, na kupelekea wanafunzi darasa la kwanza, kidato cha kwanza, na kidato cha tano kuongezeka kutoka bilioni 1 mwaka 2015 na kufikia bilioni 1.6

Waziri mkuu amesema bilioni 171 zimetumika kuimarisha miundo mbinu kujenga mabweni, nyumba za walimu 518, maabara 227, matundu ya choo 11,188 na kukarabati shule kongwe zaidi ya 75.

Ameongeza kuwa mikopo ya chuo kikuu bajeti imeongezeka kutoka billioni 348.7 na kufikia bilioni 464 kwa mwaka 2020/2021. sambamba na hilo idadi ya wanafunzi kujiunga na chuo imeongezeka kutoka 98,300, 2014/2015 na kufikia wanafunzi 104.5000 mwaka huu.

Toka Bodi ya mikopo ilipoanza serikali imetumia Tirioni 4.5 kwaajili ya mikopo ya elimu ya juu ambayo imewanufaisha sana watanzania zaidi ya laki tano.

Michelle Obama amshambulia Rais Trump
CCM yaanza mchujo wa wagombea