Kiungo kutoka nchini England Michael Carrick, ameeleza mustakabali wake ndani ya kikosi cha Man Utd kwa kusema huenda msimu huu ukawa wa mwisho kuitumikia klabu hiyo ya Old Trafford.

Carrick, mwenye umri wa miaka 35, amekua na mazingira magumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya utawala wa meneja Jose Mourinho ambaye ameonyesha kumuamini kupita kiasi kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba.

Kiungo huyo aliyesajiliwa na Man Utd akitokea Spurs mwaka 2006, ameeleza mustakabali wake alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports.

“Hakuna anayepinga kuhusu ubora wa Man Utd, lakini ninaamini umefikia wakati wa kuondoka klabuni hapo kutokana na mazingira yanayoendelea kunibana nisicheze soka, kama ilivyokua kwenye matarajio yangu.

“Nimekuwa na wakati mgumu japo natambua bado nina uwezo wa kucheza soka la ushindani, Sizungumzia vibaya kuhusu maamuzi ya meneja, lakini ipo haja kwa kila mchezaji kucheza kwa nafasi yake.

“Kwa sasa nina umri wa miaka 35, labda sababu ya umri huu ndio kikwazo kwangu, lakini siamini kwa asilimia 100 suala hilo, kwani uwezo wa kucheza ndio unaozingatiwa zaidi.”

“Ninakuhakikishia kwamba msimu huu huenda ukawa wa mwisho kwangu kuitumikia Man Utd, na kama itawezekana nitajiunga na klabu nyingine yoyote ambayo itakua tayari kunisajili.” Alisema Carrick

Samir Nasri Aendelea Kumzungumza Guardiola
Meya aliyeshiriki kumfananisha mke wa Obama na Sokwe ‘ajitumbua’