Mwigizaji maaarufu wa Marekani aliejulikana kupitia tamthiliya ya The Wire   Michael K. Williams amefariki Dunia, akiwa nyumbni kwake Broonklyn New York.

Taarifa ya kifo cha Williams imethiibitishwa na familia yake, pia majirani wameeleza kuwa baada ya kutomuona kwa siku kadhaa, walikwenda nyumbani kwake kumjulia hali siku ya jana Jumatatu na kumkuta tayari amefariki.

Aidha Vyombo kadhaa vimeripoti kuwa nyota huyo amefariki baada ya kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya (Drug Overdose) ambavyo vilikutwa nyumbani kwake mezani.

Williams amefariki Dunia akiwa na umri miaka 54.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 7, 2021
Aweso: 'RUWASA lazima tuwe wa kisasa zaidi'