FIFA iliwafungia Michel Platini na Sepp Blatter kujihusisha na soka baada ya wote wawili kukutwa na kosa la kujihusisha na mambo ya rushwa yenye thamani karibia $2m kwenye soka.

Habari mpya ni kwamba Platini amesema hajakubaliana na ishu ya yeye kufungiwa miaka 8 asijihusishe na soka kwasababu yeye ni msafi. Platini amesema kwamba hausiki hayo makosa na aliyemletea matatizo yote ni Blatter.

“Sijafanya chochote kibaya na sina wasi wasi, ni Blatter ndie ameniweka kwenye haya matatizo. Yeye ndiye mhusika na sio mimi. Kuna mtu akishirikiana na Blatter ndio wamesababisha haya yote. Ninapanga kukata rufaa”.

Kamati ya FIFA ina uwezo wa kusikiliza rufaa ya Platini lakini pia ina uwezo wa kupungaza adhabu au kuongeza zaidi.

Viingilio Vya Game Ya Simba Na Yanga Vyatangazwa
Soka La Bongo Lamuweka Jamal Malinzi Katika Mtihani Mzito